• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema Marekani haikuzingatia maendeleo ya China katika kulinda haki miliki za ujuzi

    (GMT+08:00) 2018-04-24 16:45:24

    Mkurugenzi wa Idara ya haki miliki za ujuzi ya China Bw. Shen Changyu leo hapa Beijing amesema, matokeo ya uchunguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya biashara ya Marekani hayakuzingatia au yamepuuza ukweli wa China katika kuimarisha ulinzi wa haki miliki za ujuzi.

    Amesema katika miaka ya karibuni, China imeimarisha nguvu ya kulinda haki miliki za ujuzi bila kusita, na imekuwa ikichukua msimamo mmoja katika kulinda haki miliki za ujuzi za kampuni za ndani na nje ya nchi, hatua ambayo imesifiwa na jumuiya ya kimataifa.

    Bw. Shen pia amesema, siku zote China imelipa ada ya matumizi ya haki miliki za ujuzi kwa mujibu wa kanuni za biashara ya kimataifa, ambapo mwaka jana ada ya jumla ilifikia dola za kimarekani bilioni 28.6, kati ya hizo, malipo ya China kwa Marekani yaliongezeka kwa asilimia 14.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako