• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa SCO wafikia makubaliano muhimu

    (GMT+08:00) 2018-04-24 18:32:03

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO umeamua mafanikio makuu yatakaopatikana kwenye mkutano wa kilele wa Jumuiya hiyo utakaofanyika mwezi Juni huko Qingdao, na kuweka msingi imara wa kuufanikisha mkutano huo.

    Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi nane wanachama wa Jumuiya hiyo wamebadilishana maoni kuhusu kuendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo kwenye sekta mbalimbali pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa yanayofuatiliwa na pande zote na pia wamefikia makubaliano kadhaa na kusaini nyaraka 14.

    Bw. Wang amesema, nyaraka nyingi zilizosainiwa ni miswada ya makubaliano itakayopelekwa kusainiwa au kupitishwa kwenye mkutano wa kilele wa SCO wa Qingdao, ikiwa ni pamoja na Azimio la Qingdao la Baraza la viongozi wa nchi wanachama, makubaliano ya ujirani mwema wa kudumu ya nchi wanachama na mwongozo wa utekelezaji wa miaka mitano ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako