• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Kigwangalla ataka watalii wafike mil 5

    (GMT+08:00) 2018-04-24 20:29:28

    Serikali imejiwekea mikakati itakayosaidia kuongeza idadi ya watalii nchini kupitia utangazaji wa vivutio vyake katika nchi mbalimbali zikiwamo Israel, Omani, Urusi na nchi za kusini Mashariki mwa bara la Asia.

    Akizungumza jijini Dar es Salaam, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Khamis Kigwangalla alisema hajafurahishwa na kasi ya ongezeko la watalii nchini kwa miaka kadhaa iliyopita.

    Dk Kigwangalla alisema idadi ya watalii katika miaka minne iliyopita imekuwa ni kati ya watalii 70,000 hadi 100,000, kasi ambayo hajafurahishwa nayo.

    Alisema angependa kiwango cha watalii kiongezeke kutoka milioni 1.3 hadi milioni tatu kwa miaka michache ijao.

    Naye mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Audax Mabula alisema maandalizi yameanza na wanaangalia timu itakayoshiriki katika matamasha mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako