Shilingi ya Kenya Jumanne iliendelea kuimarika dhidi ya dola ya kimarekani kutokana na mapato kutoka kwa makampuni ya ujenzi ya kigeni
Takwimu kutoka Benki Kuu ya Kenya ilionyesha shilingi Jumanne ilibadilishwa kwa dola 99.90.
Ijumaa, wiki jana shilingi ilibadilishwa kwa dola 99.95 ikiwa ni utendaji mzuri zaidi ndani ya miezi 13.
Shilingi ilio imara ni manufaa kwa wafanyabiashara wanaoagizia bidhaa kutoka nje kwani inapunguza mwanya wa ubadilishaji.
Shilingi ya Kenya ilikuwa imara mwaka jana dhidi ya dola, ikisaidiwa hasa na fedha zinazotumwa na wakenya waishio nje ya nchi na hatua za Benki Kuu ya Kenya (CBK).
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |