• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi kuu Tanzania Bara(VPL): Mechi ya Derby, Ulinzi kuongezwa

    (GMT+08:00) 2018-04-25 08:48:38
    Zikiwa zimesalia siku tano tu kueleka mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuimarisha zaidi ulinzi.

    Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, amesema kuwa jumla ya Camera 109 zitafungwa Uwanjani kuelekea mechi hiyo inayoteka hisia za mashabiki na wadau wa soka nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

    Clifford ameeleza kuwa Camera hizo zitafungwa ili kuimarisha ulinzi na usalama ndani ya uwanja ambapo zitakuwa zinarekodi matukio mbalimbali kabla na baada ya mchezo.

    Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa Aprili 29 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako