• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ngorongoro Marathon: Wakenya wazidi kutamba

    (GMT+08:00) 2018-04-25 08:49:38
    Wanariadha wa Kenya wameendelea kutamba katika ardhi ya Tanzania baada ya kunyakuwa medali ya dhahabu kwa upande wa wanawake na wanaume katika mashindano ya Ngorongoro marathoni.

    Joseph Mbatha wa Kenya alimaliza wa kwanza katika mbio hizo za kilomita 21 akitumia saa 1:04:54, nafasi ya pili imekwenda kwa Mkenya mwingine Berdarn Mussa aliyetumia saa 1:05:09, Mtanzania Paschal Mombo ameambulia nafasi ya tatu baada ya kumaliza km 21 kwa kutumia saa 1:06:05.

    Kwa upande wa wanawake, Mkenya Monica Cherito kunyakua medali ya dhahabu baada kutumia saa 1:04:54 na kuchukua nafasi ya kwanza, akifuatiwa na Failuna Abdi wa Tanzania aliyemaliza muda wa saa 1:06:12.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako