• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China afanya ziara ya ukaguzi katika mto Yangtze

  (GMT+08:00) 2018-04-25 17:17:20

  Rais Xi Jinping wa China jana alifanya ziara mjini Yichang, mkoani Hubei ili kukagua kazi za ukarabati wa mazingira ya ikolojia ya mto Yangtze na ujenzi wa ukanda wa kiuchumi wa mto Yangtze.

  Jana asubuhi, baada ya kushuka ndege iliyompeleka mjini Yichang ikitokea Beijing, mji mkuu wa China, Rais Xi alikwenda katika eneo la viwanda la rasilimali mpya la kampuni ya Xingfa lililopo kando ya mto Yangtze, na kukagua kazi za ulinzi wa mazingira na mageuzi ya kutafuta maendeleo.

  Hivi sasa, rasilimali mpya kama vile silikoni kaboni (organosilicon) zinatengenezwa katika eneo hilo la viwanda, na miradi yote inajengwa kwa kufuata mnyororo wa viwanda mzunguko, ambapo gesi taka na maji taka zote zinaweza kutumiwa tena. Baada ya kufahamishwa hali ilivyo, rais Xi anasema,

  "Ujenzi wa ukanda wa kiuchumi wa mto Yangtze unapaswa kuzingatia ulinzi, na kutolenga uendelezaji mkubwa. Hii haimaanishi kuwa hatutaki maendeleo mapya, lakini kwanza ni lazima tutunge kanuni, na kuweka kipaumbele kwa ukarabati wa ikolojia wa mto Yangtze na kulinda mto huo unaojulikana kama mto mama, na uendelezaji unaoharibu mazingira haupaswi kufanywa. Kampuni yenu imefanya vizuri katika kazi hizo, nina matumaini kuwa mtapata mafanikio zaidi katika kutafuta maendeleo endelevu kwa njia ya kisayansi."

  Mchana, rais Xi alikwenda katika kijiji cha Xujiachong kilichoko karibu na mabwawa matatu ya Gorges katika mto Yangtze na kukagua kazi za uhamaji na maisha ya wakazi wa kijiji hicho. Wanavijiji wanaofua nguo walimwambia rais Xi kuwa zamani walifulia nguo mtoni, lakini sasa kijiji hicho kimetenga maeneo ya kufulia, na wameanza kutumia maji ya bomba na maji taka yanashughulikiwa kwa pamoja.

  Magenge matatu ya  mto Yangtze ni kituo cha mwisho alichokagua rais Xi katika ziara ya siku hiyo. Amewaambia wahandisi na wanateknolojia kuwa ustawi wa taifa unahitaji juhudi za muda mrefu bila ya kuogopa taabu. Anasema,

  "Ustawi wa taifa la China hauwezi kupatikana kwa urahisi. Tunatakiwa kufanya juhudi, na kupata mafanikio kwenye utengenezaji wa kiviwanda. Ni lazima tujitegemee na kuhimiza kuinuka kwa uwezo wa ubunifu. Mfano wakati ule tulipojenga magenge matatu, kama tungetegemea nguvu na misaada ya nchi za nje, basi tusingekuwa na uwezo wa kuongoza kama wa leo. Tulishinda taabu na matatizo, sio tu tumepata mafanikio katika mradi huo, bali pia tumepata wataalamu kama nyinyi, tunawaonea fahari, na pia tunajionea fahari kutokana na taifa letu kuwa na uwezo namna hiyo. Natarajia kuwa kutokana na juhudi zetu za pamoja na umoja, wachina bilioni 1.3 tutaweza kutimiza ndoto ya China."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako