Rais Donald Trump wa Marekani amesema, waziri wa fedha wa nchi hiyo Bw. Steven Mnuchin na mwakilishi wa biashara Bw. Robert Lighthizer wataongoza ujumbe wa Marekani kwenda China ili kujadili suala la biashara katika siku zijazo.
Hivi karibuni, wizara ya biashara ya China ilisema, China imepata habari kuwa Marekani inapenda kufanya majadiliano na China kuhusu suala la biashara, na China inakaribisha hatua hiyo ya Marekani.
Msemaji wa wizara ya biashara ya China Gao Feng hivi karibuni alisema, hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru mkubwa dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka China kwa mujibu wa uchunguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya biashara ya Marekani, imekiuka kanuni ya pande nyingi, na ni kitendo cha kujilinda kibiashara.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |