• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Bei ya maziwa yatarajiwa kupanda

    (GMT+08:00) 2018-04-25 19:22:22

    Bei ya maziwa nchini Kenya inatarajiwa kupanda ikiwa bunge la Kitaifa litapitisha mswada unaopendekeza ushuru wa asilimia moja kwa bidhaa za maziwa zinazotayarishwa nchini Kenya.

    Mswada huo maarufu kama "Statute Law (Miscellaneous Amendment) Bill 2008 utatoa nafasi kwa serikali za kaunti kuanzisha ada fulani kwa maziwa ama bidhaa zote za maziwa zinazotayarishwa katika maeneo yao.

    Mswada huo ambao unarekebisha sheria mbalimbali unapendekeza kuwa ushuru huo utaelekezwa kwa Bodi ya Maziwa Nchini (Kenya Dairy Board-KDB).

    Mswada huo uliowasilishwa bungeni na kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale unasema kila mtayarishaji wa maziwa atalipa ushuru wa asilimia moja kwa kila kilo moja ya maziwa anayouza. Ushuru huo utalipwa kwa bodi inayosimamia sekta ya maziwa nchini.

    Kampuni kuu za kutayarisha maziwa kwa sasa zinalipa wakulima Sh37 kwa lita moja ya maziwa.

    Kampuni ya Brookside iliongeza malipo yake wiki jana lakini New Kenya Cooperative Creameries (KCC) haijaongeza malipo hayo kufikia sasa.

    Hata hivyo, mabadiliko hayo yatakuwa afueni kwa wakulima kwa sababu ada ambazo wao hulipa, yaani "cess" sasa hazitakatwa na kampuni za maziwa kutoka kwa pesa wanazolipwa kila mwezi baada ya kuwasilisha maziwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako