• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madini mapya yagunduliwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-04-25 19:22:58

    Madini aina ya kinywe yaliyogundulika Tanzania ambayo hutumika hutengeneza betri,breki,na kinga za mashine hivi karibuni yataanza kutumika ulimwenguni baada ya sampuli yake tani 500 kupelekwa Canada kwa ajili ya kufanyiwa majaribio.

    Taarifa za ugunduzi wa kinywe zilitangazwa mwishoni mwa wiki na Ofisa Madini Mkoa wa Morogoro,Theresia Ntuke wakati wa uzinduzi wa usafirishaji wa madini hayo yanayopatikana Mahenge wilayani Ifakara mkoani Morogoro.

    Sampuli za madini hayo zilisafirishwa na kampuni ya uchimbaji madini ya ya Mahenge Resources kwa kutumia treni ya Tazara kutoka Ifakara kwenda Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu ya kuzipeleka Canada.

    Akizungumza na wananchi walioshuhudia usafirishaji wa madini hayo,Ntuke alisema kampuni hiyo ipo katika hatua ya upembuzi yakinifu wa utafiti wao ambao kiasi cha madini ya kinywe yaliyogunduliwa hadi sasa ni tani milioni 69.9.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako