• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ajira mpya kuzalishwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-04-25 19:23:49

    Ajira za mamia zinatarajiwa kuzalishwa nchini Tanzania baada ya Israel kuahidi kuwekeza mitaji kwenye sekta tatu ikiwemo kilimo.

    Sekta nyengine ni teknolojia ya habari na mawasiliano na ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza dawa na vifaa tiba.Kilimo pekee kinaajiri zaidi ya asilimia 80 ya watanzania takriban milioni 50 waliopo sasa hivyo uwekezaji wa Israel katika sekta hiyo unatarajiwa kunufaisha mamia.

    Matumaini hayo yalibainika jana jijini Dar es Salaam baada ya Waziri wa Viwanda,Biashara,na Uwekezaji ,Charles Mwijage kutangaza ujio wa wafanyabiashara kutoka Israel wakati akifungua kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako