• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michuano ya CECAFA U17: Serengeti Boys yatinga fainali, yaipiga Kenya

    (GMT+08:00) 2018-04-26 08:12:18
    Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na kati (CECAFA U17) baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Kenya mchezo uliochezwa jana uwanja wa Muyinga nchini Burundi.

    Haukukuwa ushindi mwepesi kwa Serengeti Boys, ililazimika kutoka nyuma kwa bao 1-0 ili kuwalaza Wakenya 2-1 baada ya dakika 90.

    Timu hiyo ya Tanzania sasa inasubiri mshindi wa mechi ya nusu fainali ya pili kati ya Uganda na Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako