• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge Tanzania kupambana na EALA

    (GMT+08:00) 2018-04-26 08:13:15
    Timu za mpira wa miguu na mikono za Bunge la Jamhuri ya Muungano (Bunge Sports) leo zinajitupa uwanjani kumenyana na wenzao wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) mjini Dodoma.

    Michezo hiyo itafanyika baada ya maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye uwanja wa Jamhuri mjini humo.

    Msemaji wa Bunge Sports, Amina Mollel amewaeleza waandishi wa habari kuwa, timu hiyo inayoundwa na wabunge kutoka vyama mbalimbali imejiandaa vya kutosha na kuahidi burudani kwa wakazi na wageni wa mkoa huo ambao kijiografia, upo katikati ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako