• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya: Real Madrid kama kawa kama dawa, yaipiga Bayern Munich, Allianz Arena

    (GMT+08:00) 2018-04-26 08:13:33

    Nusu fainali nyingine ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imepigwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Allianz Arena kwa kuzikutanisha Real Madrid ya Uhispania na Bayern Munich ya Ujerumani.

    Kuna msemo usemao "Kutangulia si kufika, na wengine husema "ujanja kupata si kuwahi" misemo hii miwili inawahusu Bayern Munich baada ya kutangulia kufunga goli kupitia kwa Josh Kimmich katika dakika ya 28 ya mchezo kabla ya Marcelo kuisawazishia Real Madrid dakika ya 44.

    Marco Asensio alishindilia msumari wa mwisho kwa Bayern Munich baada ya kuipatia timu yake Real Madrid goli la ushindi katika dakika ya 57.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako