• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa SCO watoa taarifa ya pamoja

    (GMT+08:00) 2018-04-26 09:56:53

    Taarifa ya pamoja ya Mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai SCO ilitolewa jana.

    Katika mkutano huo uliofanyika Jumanne mjini Beijing, mawaziri hao walibadilishana maoni juu ya hali ya kimataifa na kikanda, kukuza ushirikiano wa kiutendaji kwenye mambo ya ulinzi na usalama kati ya nchi wanachama na masuala mengine yanayofuatiliwa kwa pamoja.

    Mawaziri hao wamesisitiza kuwa amani na maendeleo bado ni mwelekeo wa zama za sasa, wakati machafuko na hali zisizotabirika duniani vinaongezeka.

    Pia wamekubaliana kuwa mapambano dhidi ya ugaidi, itikadi kali na ufarakanishaji, na kuimarisha amani, usalama na utulivu wa kikanda ni vipaumbele kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako