• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Bei ya umeme kupunguzwa kuanzia mwezi ujao

    (GMT+08:00) 2018-04-26 19:06:39

    Gharama ya umeme itapunguzwa kuanzia mwezi ujao.

    Waziri wa kawi nchini Kenya Charles Keter amesema kampuni ya usambazaji umeme nchini Kenya Kenya power, itabadilisha tariff zake kwa ajili ya kushukisha bei.

    Katika kongamano la magavana linaloendelea katika kaunti ya Kakamega ,Keter amesema bei ya umeme kwa mwanachi wa kawaida itapunguzwa kwa asilimia 30.

    Haya yanajiri kufuatia malalamishi ya wakenya wengi kuhusiana na bei hizo kupanda maradufu.

    Hata hivyo haijabanishwa haswa viwango vya ununuzi wa umeme lakini wateja wanaotumia baina ya uniti 1 hadi 50 watapunguziwa bei na wale wanaotumia uniti zaidi ya 50 hadi elfu moja watakuwa na bei zao tofauti.

    Kampuni ya Kenya Power itaweka bei tofauti katika kila kaunti kulingana na ubora wa huduma hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako