• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Hali ya uchumi wa Kenya ngumu

    (GMT+08:00) 2018-04-26 19:07:21

    Idadi kubwa ya wakenya wamekabiliwa na umaskini mwaka 2017 ikilinganishwa na mwaka 2016 kwa mujibu wa utafiti wa uchumi na data za shirika la kitaifa la takwimu.

    Sababu zilizochangia hali ngumu za maisha ni pamoja na bei ya juu ya bidhaa pamoja na ukosefu wa nyongeza za mishahara kutoka kwa waajiri.

    Utafiti wa uchumi wa mwaka 2018 unaonyeshwa kwamba kipato cha wastani cha wafanyikazi kilishuka kwa elfu moja kutokana na kupanda kwa ushuru.

    Kupanda kwa bei ya mafuta aidha kumetajwa kusababisha mfumko wa uchumi uliopandisha gharama ya maisha kwa viwago vikubwa.

    Katika ripoti hiyo,mfumko wa uchumi ulipanda hadi asilimia 6.8 .

    Waziri wa fedha Henry Rotich ana matumaini kwamba mwaka huu maisha ya wakenya ya uchumi yataboreka kufuatia mvua inayoendelea kunyesha .

    Kenya inatarajia kushuhudia ongezeko la mavuno na uzalishaji bora utakaofikisha ukuwaji wa uchumi asilimia 5.8 kutoka 4.9.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako