• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Wanaouza mafuta ya petrol bila leseni kufungwa jela

    (GMT+08:00) 2018-04-26 19:07:42

    Wizara ya kawi na petroli nchini Uganda imetoa onyo kwa vituo vya kuuza mafuta vinavyoendesha biashara hiyo bila leseni.

    Zaidi ya vituo 114 vimethibitishwa kuuza mafuta ya petroli na bidhaa nyingine kinyume na sheria na tayari wamepokonywa leseni.

    Hatua hii ni baada ya serikali kugundua kwamba ushuru wa uuzaji wamfuta umepungua kwa asilimia 0.5 mwaka 2018 .

    Takwimu kutoka kwa wizara ya kawi zinaonyesha kwamba, kumekuwa na wafanyibiashara wengi wanaoagiza mafuta na kusafirisha mafuta nje na ndani ya nchi bila ya kufuata sheria ya mafuta iliyowekwa mwaka 1999.

    Kwa sasa oparesheni ya kubaini vituo sahihi vya mafuta Uganda imevipata zaidi ya vituo 2000 na hatia ya kutofikia viwango vya serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako