• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania;Gesi asilia kutumika majumbani

    (GMT+08:00) 2018-04-26 19:08:38

    Serikali ya Tanzania itaanza kusambaza gesi asilia kwa matumizi ya majumbani na viwandani baada ya kukamilika kwa miundombinu ya kusambaza gesi hiyo miezi miwili ijayo.

    Usambazaji huo unafuatia hatua ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), kukabidhi kwa mkandarasi mradi wa uunganishaji wa miundombinu ya taifa ya gesi asilia kwenye bomba la usambazaji la Ubungo-Mikocheni jijini Dar es Salaam.

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Kapuulya Musomba amesema mradi huo ambao ni awamu ya kwanza, unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi miwili n utagharimu kati ya Sh bilioni 4 hadi 5 na baada ya hapo utaratibu wa kuwaunganishia wateja utaanza.

    Kiwango hicho cha mgandamizo kimeelezwa kuwa ni kikubwa hivyo mkandarasi atajenga kituo kingine cha kupunguza mgandamizo huo wa gesi asilia hadi kufikia bar 7 jirani na BVS 15. Ili gesi hiyo iweze kutumika viwandani na majumbani bila kuleta madhara, imeelezwa kuwa itapunguzwa tena hadi kufikia mgandamizo mdogo wa bar 4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako