• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kupunguza zaidi muda mzunguko wa mapitio ya chapa ya biashara kabla ya kuisajili

    (GMT+08:00) 2018-04-27 16:31:33

    China inatarajia kupunguza zaidi muda wa mapitio ya chapa za biashara hadi kufikia muda wa usiozidi miezi minne na kuboresha huduma zake za usajili wa biashara katika kipindi cha kufikia mwaka 2020.

    Maombi ya kusajili biashara nchini China yalifikia karibu milioni 5.75 mwaka 2017 kutokana na ongezeko la shughuli za ujasiriamali na uvumbuzi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 55.7 kwa mwaka huo.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na makamu mkurugenzi wa Ofisi ya Idara ya taifa ya usimamizi wa masuala ya Biashara (SIPO), Bw. Chen Wentong, ili kufanikisha zoezi la kusajili biashara, mamlaka zinazohusika zinapaswa kuboresha mifumo itakayowasaidia wafanyabiashara na umma kwa ujumla.

    Katika mpango wa miaka mitatu ulioanza kutekelezwa mwezi Machi mwaka huu, SIPO iliweka nadhiri ya kuboresha usajili wa biashara kwa kuboresha utendaji katika mapitio, kurahisisha njia za kujisajili, kuboresha msaada wa kitaalamu na kuhimiza ulinzi wa sheria za kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako