• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hali ya utoaji wa nafasi za ajira ya China yapata maendeleo katika robo ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-04-27 17:18:39

    Msemaji wa wizara ya raslimali watu na huduma za jamii ya China Bw. Lu Aihong amesema, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, hali ya utoaji wa nafasi za ajira imepata maendeleo nchini China. Siko la ajira linaendelea kuchangamka huku mahitaji ya nguvukazi ya sekta ya utengenezaji yakiendelea kuwa imara.

    Katika robo ya kwanza ya mwaka huu, nafasi mpya za ajira ziliongezeka kwa watu milioni 3.3 katika miji na wilaya nchini China, huku kiwango cha ukosefu wa ajira kikifika asilimia 3.89, ambacho kimepungua kwa asilimia 0.08 ikilinganishwa na mwaka jana. Bw. Lu Aihong amesema, soko la ajira katika robo ya kwanza ya mwaka huu limetoa ishara nzuri. Anasema,

    "sababu ni kuwa mahitaji ya nguvukazi bado hayajapungua. Takwimu zilizotolewa na mashirika ya kuhudumia utoaji wa nafasi za ajira kwa umma katika miji 100 zinaonesha kuwa soko la ajira limeonesha uhai mkubwa, ambalo idadi ya nafasi za ajira ni kubwa kuliko idadi ya watu wanaotafuta ajira. Mbali na hayo, mahitaji ya nguvukazi ya sekta ya utengenezaji yanaendelea kuongezeka, ambayo yalikua kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na mwaka jana. "

    Kigezo cha ajira ni kigezo cha msingi cha kutathmini maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Bw. Lu amesema, takwimu za robo ya kwanza ni nzuri kutokana na mchango wa mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uchumi wa taifa. Anasema,

    "Katika robo ya kwanza, pato la taifa liliongezeka kwa asilimia 6.8 ikilinganishwa na mwaka jana, maagizo kutoka nje na mauzo kwa nje pia yalikuwa ya kasi. Hasa kutokana na mageuzi ya mfumo wa mambo ya kibiashara, nguvu mpya ya kuhimiza maendeleo inaendelea kuimarika. Katika robo ya kwanza, idadi ya kampuni mpya zilizoandikishwa imefikia milioni 1.32 ambazo zinaendelea kutoa mchango katika soko la ajira."

    Bw. Lu pia amesema, mwaka jana idadi ya nguvukazi mpya itazidi milioni 15, shinikizo la utoaji wa nafasi za ajira bado ni kubwa. Serikali ya China itazidi kufanya juhudi, ili kutimiza malengo ya ajira na kuhakikisha utulivu kwenye soko la ajira,. Anasema,

    "katika hatua ijayo, china itaendelea kutekeleza mkakati wa kutoa kipaumbele kwenye nafasi za ajira, kuweka sera chanya za ajira na kutilia maanani kufanya juhudi kwenye utoaji wa nafasi za ajira, kusaidia kujiajiri, kuhimiza huduma, kuzuia changamoto, ili kuhakikisha kukamilika kwa malengo na utulivu wa hali ya jumla. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako