• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • John Finley kusitisha uzalishaji wa maua Kericho

  (GMT+08:00) 2018-04-27 18:54:08

  Kampuni ya Uingereza ya John Finley inayojihusisha na kilimo cha maua imetangaza mpango wa kusitisha uzalishaji wa zao hilo kwenye mashamba yake mjini Kericho. Hatua ya kampuni hiyo huenda ikawafanya watu elfu 2 kukosa ajira. John Finley ambayo pia miongoni mwa makampuni yanayozalisha chai na kuuza nje imesema hatua hiyo inatokana na kupanda kwa gharama ya uzalishaji katika eneo hilo la Kericho.

  Taarifa kutoka kwa kampuni hiyo imesema inasikitishwa na hatua waliochukua.Kampuni hiyo pia inamiliki mashamba katika eneo la Naivasha pamoja na eneo la mlima Kenya. Hata hivyo imesisitiza kuwa shughuli katika mashmba mengine zitaendelea kama kawaida. Mpango wa kufunga shughuli kwenye mashamba ya Kericho utafanywa kwa awamu. Taarifa ya kampuni hiyo inakuja miaka miwili tu baada ya mahakama ya wafanya kazi nchini Kenya kutoa hukumu ya kuwapa wafanya kazi wa kampuni hiyo pamoja na wa Uniliver nyongeza ya mshahara ya asilimia 30.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako