• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AFDB kusaidia utekeleza wa miradi Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-04-27 18:54:28

    Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo inayogusa maisha ya wananchi kama upatikanaji wa uhakika wa nishati ya umeme.

    Akizungumza baada ya kutembelea kituo cha Kupooza Umeme cha Zuzu, mkuu wa Benki hiyo, Dk Akinwumi Adesina amesema AfDB imesaidia kujenga njia ya umeme wa KV 400 kutoka Iringa - Shinyanga kupitia Dodoma na Singida kwa dola za Marekani milioni 64. Dk Adesina ameongeza kuwa Tanzania imeongeza uwezo wa kuzalisha umeme kwa wananchi kutokana na ushirikiano wake na wadau mbalimbali wa nje.

    Amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo nchini humo.

    Kwa upande wake, naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu amesema, AfDB imesaidia ujenzi wa njia hiyo ya umeme na vijiji 121 kuunganishwa msongo wa KV 400.

    Alisema AfDB inatekeleza miradi mbalimbali na matarajio ya Serikali ni kuona benki hiyo inashiriki katika miradi mbalimbali iliyopo. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango aliishukuru AfDB kwa kusaidia mradi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako