• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yatengeneza mwavuli wa kuzalisha umeme kwa Waafrika

    (GMT+08:00) 2018-04-28 15:10:06

    Kampuni ya Hanergy ya China imetangaza mradi wa hisani wa kutengeneza mwavuli wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua unaolenga kuwanufaisha watu wa nchi za Afrika wasiopata huduma za umeme.

    Hayo yametangazwa na mkuu wa kampuni hiyo anayeshughulikia mauzo katika nchi za nje Bw. Lyu Yuan kwenye kituo cha maonesho ya nishati safi cha makao makuu ya kampuni hiyo.


    Bw. Lyu ameeleza kuwa mwavuli huu wenye uzito wa kilo 9 unaweza kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua, kulimbikiza umeme wa mA elfu 40, kuwasha taa kwa saa 10, na kukidhi mahitaji ya watoto 8 hadi 10 ya kupata taa ya kusoma, au mahitaji ya familia 10 ya kuchaji simu za mkononi.

    Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watu wasiopata huduma za umeme barani Afrika imefikia milioni 880, na ni asilimia 55 ya watu wote wasio na huduma za umeme duniani. Wakati huo huo, Afrika ina maliasili kubwa ya jua ambayo nishati yake haijatumiwa vizuri.

    Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Hanergy Bw. Li Hejun amesema, jina la mwavuli huo ni Humbrella, maana yake ni mwavuli wa matumaini. Kampuni yake inataka kuchangia maendeleo ya Afrika kwa kutumia teknolojia zake.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako