• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga ripoti maalum ya namba 301 ya Marekani

    (GMT+08:00) 2018-04-28 19:05:23

    Mkuu wa idara ya sheria ya wizara ya biashara ya China leo amejibu ripoti maalum ya namba 301 iliyotolewa na ofisi ya wajumbe wa biashara wa Marekani kuhusu hakimiliki ya ujuzi. Amesema katika muda mrefu uliopita, Marekani ilishutumu na kulaani hali ya hakimiliki ya ujuzi ya nchi nyingine kwa upande mmoja, na haina vigezo halisi na usawa, na ilipingwa na nchi husika.

    Mkuu huyo alidhihirisha kuwa, katika ripoti hiyo, Marekani ilipuuza ukweli na kuendelea kuiweka China kwenye orodha ya nchi zinazopaswa kuchunguzwa. China inakipinga kitendo cha Marekani na kuitaka Marekani itekeleze ahadi ya pande mbili kati ya China na Marekani, kuheshimu ukweli, na kutathimini kwa haki na usawa juhudi na mafanikio ya serikali za nchi nyingine ikiwemo China katika sekta ya hakimiliki ya ujuzi.

    Habari nyingine zinasema, kwenye mkutano wa idara ya WTO inayoshughulikia mvutano wa kibiashara, China imetoa maoni kwamba, ripoti ya namba 301 ni tishio la mfumo wa kibiashara wa pande nyingi, na kutaka nchi wanachama wa WTO kuipinga kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako