• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China na India waafikiana kuhusu mambo mbalimbali

    (GMT+08:00) 2018-04-28 19:06:43

    Rais Xi Jinping wa China jana na leo mjini Wuhan, China amefanya mkutano usio rasmi na waziri mkuu wa India Bw. Narendra Modi. Viongozi hao wawili wamebadilishana maoni kwa kina kuhusu hali ya kimataifa, uhusiano kati ya nchi hizo mbili, mustakabali wa maendeleo ya nchi zao, na sera za ndani na za kimataifa, na kufikia makubaliano mengi.

    Viongozi hao wamekubaliana kuwa hali ya kimataifa inabadilisha kwa kina, nguvu za kimataifa zina uwiano zaidi, na mwelekeo wa jumla wa amani na maendeleo haubadiliki, wakati huo huo dunia bado inakabiliwa na hali za kutatanisha. Wanaona kuwa China na India zote ni nchi kubwa zinazoendelea zenye idadi kubwa ya watu na historia ndefu. Nchi hizo mbili zikidumisha uhusiano wenye amani, utulivu na uwiano zitasaidia utulivu wa dunia. Zinapaswa kutoa mchango kwa ajili ya amani na maendeleo ya dunia.

    Viongozi hao pia wamekubaliana kuendelea kudumisha mawasiliano ya kimkakati kwa njia tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako