• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simba yashinda kwa goli 1-0 dhidi ya Yanga mjini Dar es Salaam

    (GMT+08:00) 2018-04-30 10:09:57

    Katika mechi ya watani wa jadi wa kihistoria Afrika Mashariki ngazi ya klabu, Simba imepata ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga, mjini Dar es Salaam nchini Tanzania.

    Goli la Simba lilipatikana kunako dakika ya 37 kupitia beki wake Erasto Nyoni aliyefunga kwa kichwa kutokana na krosi iliyopigwa na Shiza Ramadhani Kichuya.

    Licha ya kuingia kwenye historia ya utani wa jadi, Ushindi huu pia unaifanya simba ifikishe pointi 62, na ni mazingira mazuri kuelekea ubingwa ikiwa imesaliwa na mechi 4 mkononi.

    Yanga inasalia katika nafasi ya 3 ikiwa na pointi 48 nyuma ya Azam FC yenye 49, na ikiwa imesalia na mechi 4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako