• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais AfDB aiahidi neema Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-04-30 19:54:26

    RAIS wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk Akinumwi Adesina amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini na kuahidi atahakikisha Tanzania inaendelea kunufaika na misaada na mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kisasa katika Jiji la Dodoma na mradi wa kuzalisha umeme.

    Dk Adesina amemmwagia sifa Rais John Magufuli kwa namna anavyosimamia ukuaji wa uchumi uliofikia wastani wa asilimia 7 kwa mwaka.

    Pia kwa kupambana na vitendo vya ufisadi, rushwa, kuimarisha uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi, kupiga vita matumizi mabaya ya rasilimali za umma ili kuwaondoa wananchi wake katika umasikini.

    Aidha, alimtambua Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, kwa kusimamia uchumi na sera ya bajeti na fedha, kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha ili nchi ipige hatua kubwa kupitia miundombinu inayotekelezwa na AfDB na washirika wengine wa maendeleo.

    Miongoni mwa miradi ambayo benki hiyo imepanga kusaidia ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa utakaojengwa Msalato nje kidogo ya Jiji la Dodoma ambapo kwa kuanzia benki hiyo itatoa zaidi ya Sh bilioni 200.

    Tanzania imeshika nafasi ya pili katika Bara la Afrika kwa ukuaji wa uchumi kwa kasi ikitanguliwa na nchi ya Ethiopia.

    Ushirikiano wa AfDB na Tanzania ulianza tangu mwaka 1971, ambako mpaka sasa benki hiyo imewekeza kiasi cha dola bilioni 3.6, sawa na zaidi ya Sh trilioni 8, katika miradi mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo umeme, barabara, maji na usafi wa mazingira, uboreshaji rasilimali watu pamoja na masuala ya utawala bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako