• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dominica yatangaza kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China

    (GMT+08:00) 2018-05-01 18:39:51

    Jamhuri ya Dominica jana usiku imetangaza kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China.

    Mshauri wa serikali ya Dominica, Bw. Flavio Dario Espinal amesema, serikali imetoa uamuzi huo baada ya kufikiria kwa muda mrefu na kufanya majadiliano na nyanja za siasa na biashara, na pia uamuzi huo unafuata mahitaji ya watu wa Dominica na mustakabali wa maendeleo ya nchi hiyo. Amesema Jamhuri ya Dominica inashikilia msimamo wa kuwepo kwa China moja duniani na Taiwan ni sehemu ya China isiyotengeka.

    Habari zinasema, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na mwenzake wa Dominika Miguel Vargas Maldonado, leo wamesaini rasmi azimio la pamoja la kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati yao mjini Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako