• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini: MTN kupanua huduma Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-05-01 18:57:32

    Kampuni ya mawasiliano ya MTN ya Afrika Kusini imeahidi kupanua huduma zake hadi Sudan Kusini ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka nchini humo.

    Mkuu wa mawasiliano wa kampuni hiyo nchini Sudan Kusini Khumbulani Dhlomo, hata hivyo amesema wanakabiliana na changamoto kadhaa hasa kutokana na mgogoro wa kisiasa wa muda mrefu.

    Dhlomo amesema changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa usalama na hali mbaya ya kiuchumi

    MTN yenye wateja 800, 000 ilitumia dola milioni $170 kwenye soko la Sudan Kusini kuanzia mwaka wa 2014 na 2015 lakini haijawahi kupaa faida.

    MTN ndio ya pili kwa ukubwa wa kampuni za mawasiliano Sudan Kusini baada ya Vivacell.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako