• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Morocco: Benki ya Dunia na IMF kufanya mkutano mkuu Morocco 2021

    (GMT+08:00) 2018-05-01 19:00:13

    Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF) zinatarajia kufanya mkutano wake mkuu mwaka 2021 nchini Morocco.

    Uamuzi wa kufanyia mkutano huo jijini Marrakech umetokana na kura zilizopigwa na jopo la magavana wa taasisi hizo.

    Mara ya mwisho taasisi hizo kufanyia mkutano wake Afrika ilikuwa jijini Nairobi, mwaka 1973.

    Mkutano huo wa mwaka huwakutanisha magavana wa benki kuu, mawaziri wa fedha, wakurugenzi wa kampuni binafsi, asasi za kiraia, vyombo vya habari na wasomi wa masuala ya fedha, uchumi na maendeleo.

    Mkutano huo utakaofanyika Oktoba 2021 ujadaili masuala kadhaa ya kidunia ukiwami mwenendo na ustawi wa uchumi, vita dhidi ya umasikini, utengenezaji wa nafasi za ajira na mabadiliko ya tabianchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako