• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatekeleza sheria mpya kadhaa kuanzia tarehe mosi Mei

    (GMT+08:00) 2018-05-02 16:52:48

    Kuanzia tarehe mosi, Mei, sheria mpya kadhaa zimeanza kutekelezwa nchini China. Sheria hizo ni pamoja na sheria ya kuwaenzi mashujaa waliofariki kutokana na maslahi ya umma, sheria ya kusamehe ushuru wa forodha kwa baadhi ya dawa kutoka nchi za nje, na mapendekezo ya kupiga marufuku watu wasio na maadili kusafiri kwa ndege na treni.

    Sheria iliyopitiwa hivi karibuni na baraza la kudumu la bunge la umma la China ya kuwaenzi mashujaa waliofariki kutokana na maslahi ya umma imeanza kutekelezwa rasmi. Kwa mujibu wa sheria hiyo, nguvu ya kulinda haki za majina, picha, heshima na sifa itaongezeka. Profesa Lyu Jingsheng wa Chuo Kikuu cha Umma cha China anasema,

    "Sheria hiyo ni ya kiutawala. Si kama tu inaweza kulinda maslahi ya mashujaa waliofariki kwa ajili ya maslahi ya umma, bali pia inahakikisha maslahi ya umma na utaratibu wa jamii kwa kudumisha mawazo safi kuhusu thamani. Ni sheria muhimu sana."

    Katika upande wa maisha ya wananchi, kuanzia tarehe mosi, Mei, China imechukua hatua mbalimbali ili kupunguza matatizo ya kupata matibabu. Naibu mkurugenzi wa baraza la afya la China Bw. Zeng Yixin anasema,

    "Kuanzia tarehe mosi, Mei mwaka huu, China itasamehe ushuru wa forodha wa baadhi ya dawa zinazoagizwa kutoka nje, zikiwemo dawa za mitishamba ya kichina na dawa za saratani. China pia imetoa hatua ya kupunguza ushuru mwingine wa dawa hizo, zikiwemo aina 103 za dawa za saratani."

    Kuharakisha ujenzi wa jamii yenye uaminifu ni msingi muhimu wa kujenga jamii yenye masikilizano ya kijamaa. Kuanzia tarehe mosi, Mei, China itatekeleza mapendekezo mawili yaliyotolewa na kamati kuu ya maendeleo ya mageuzi ya China, ofisi ya ustaarabu ya China pamoja na idara nyingine sita za serikali. Kutokana na mapendekezo hayo, kwa muda fulani, watu waliofanya udanganyifu katika madeni watapigwa marufuku kusafiri kwa treni, huku watu waliofanya vurugu kwenye ndege wakipigwa marufuku kusafiri kwa ndege, ili kuhimiza ujenzi wa jamii yenye uaminifu.

    Mbali na hayo, sheria ya muda kuhusu mashirika ya kufikisha vifurushi kwa haraka, na utaratibu mpya wa kuomboa pasipoti pia zimeanza kutekelezwa tarehe mosi Mei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako