• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bustani za mji wa Beijing zapokea wageni zaidi ya milioni moja wakati wa mapumziko ya Siku ya Wafanyakazi Duniani

    (GMT+08:00) 2018-05-02 18:15:41

    Zaidi ya watu milioni 1.9 walitembelea bustani 11 zilizopo kwenye manispaa ya Beijing na Bustani za Makumbusho za China wakati wa mapumziko ya siku tatu ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyoanza jumapili ya tarehe 29 mwezi uliopita.

    Kituo cha Usimamizi wa Bustani katika Manispaa ya Beijing kimesema, bustani tatu zilizoongoza kwa kutembelewa zaidi ni Summer Palace, Bustani ya Wanyama ya Beijing, na Bustani ya Beihai. Karibu maonyesho 20 ya kitamaduni yalifanyika mjini Beijing, na baadhi ya maonyesho hayo yataendelea mpaka mwisho wa mwezi huu, ikiwemo maonyesho ya maua katika bustani kadhaa ikiwemo Bustani ya Zhongshan, Bustani ya Jingshan, na Bustani ya Xiangshan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako