• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Uwanja wa KIA kupokea ndege kubwa zaidi,na kuongeza idadi ya watalii nchini

    (GMT+08:00) 2018-05-02 19:21:27

    Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ,umejipanga kupokea ndege kubwa zinazoleta watalii ili kukuza sekta hiyo.

    Watalii wengi wanaoshuka uwanjani hapo hutembelea vivutio vilivyopo mkoani Arusha ,manyara,na Serengeti ,mkoani Mara.

    Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya Maendeleo ya Kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro ,(KADCO),Mhandisi Ande Mkoma alisema hayo wakati akijibu swali kutoka kwa waandishi wa habari Arusha.

    Alisema ndege kubwa ya Australia Boeing 747-400 Qantas ilitua wiki iliyopita katika uwanja huo ikiwa na watalii 380 kutoka nchini humo.

    Aidha alisema uwanja huo una uwezo wa kupokea ndege ya ukubwa wowote kutokana na maboresho yaliyofanywa katika uapna na urefu wa njia ya kuruka na kutua ndege,kuweka vifaa muhimu na kuboresha huduma.

    Uwanja huo ambao ulijengwa mwaka 1971 upo katikati ya Moshi na Arusha,na umekuwa ukitoa huduma kwa abiria wapatao 900 kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako