• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Turkana waitaka serikali kuwapatia mgao wa asilimia 10 ya rasilimali ya mafuta

    (GMT+08:00) 2018-05-02 19:22:03

    Viongozi wa kisiasa kutoka kaunti ya Turkana nchini Kenya wametoa kauli ya pamoja kuwa hawataruhusu usafirishaji wa mafuta kutoka eneo hilo hadi serikali itakapowahakikishia kuwa jamii hiyo itapewa asilimia 10 ya mapato kutokana na mauzo ya bidhaa hiyo.

    Wakiongea mjini Lokichar,viongozi hao wakiwemo Gavana Josphat Nanok, Naibu Gavana Peter Lotethiro, Seneta Malachu Ekal, Mbunge wa Turkana Kusini James Lomenen, Mohammed Ali Lokuru (Mbunge wa Turkana Mashariki) na madiwani 11 waliishutumu serikali kwa kusimamishwa kwa muda mrefu kwa mswada wa Petroli wakisema hatua hiyo haikuwa na nia njema.

    Gavana Nanok alisema wanamkashifu Kiongozi wa Wengi Bungeni Aden Duale kwa hatua hiyo ambayo ililenga kuwanyima haki yao ya kupata mgao wa mapato kutoka kwa rasilimali hiyo ambayo iko eneo lao.

    Alisema viongozi hao wataungana hadi pale Turkana itakapopata mgao wake wa mapato kutokana na mauzo ya mafuta kufidia miaka mingi ambayo kaunti hiyo imetengwa kimaendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako