• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya kibiashara yanaendana na maslahi ya pamoja ya China na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-05-02 20:52:40

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, kutatua migongano kwa kupitia mazungumzo kunaendana na maslahi ya pamoja ya China na Marekani.

    Bibi Hua Chunying amesema, China na Marekani zikiwa ni nchi kubwa kiuchumi duniani zinapaswa kutatua migongano kwa kupitia mazungumzo na kulinda hali ya ujumla yenye utulivu ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili. Amesema hatua hiyo inaendana na maslahi ya pamoja ya China na Marekani, pia ni matarajio ya pamoja ya nchi mbalimbali duniani, kuna umuhimu mkubwa kwa ufufuzi na utulivu wa uchumi wa dunia.

    Ujumbe wa Marekani unaoongozwa na waziri wa mambo ya fedha wa Marekani Steven Mnuchin utafanya ziara nchini China kuanzia kesho, na naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He atabadilishana maoni na wajumbe wa Marekani kuhusu masuala ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako