• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ligi Kuu ya Rwanda: Klabu ya Kiyovu kuchunguzwa kwa kudaiwa kutoa rushwa ili kushinda mechi

    (GMT+08:00) 2018-05-03 08:55:56

    Shrikisho la mpira wa miguu nchini Rwanda FERWAFA limeanzisha uchunguzi dhidi ya klabu ya Kiyovu inayoshiriki ligi kuu baada ya kuwepo madai ya kutoa rushwa ili kupata ushindi kwenye mechi dhidi ya Miroplast wiki iliyopita.

    Kocha mkuu wa Miroplast Suleiman Niyibizi alitoa malalamiko kuwa wachezaji wake walilipwa pesa na Kiyovu ili wakubali kufungwa na ndiyo maana wakafungwa magoli 2-0, jambo ambalo FERWAFA imeanza kulifanyia uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuwahoji baadhi ya wahusika wakiwemo waamuzi wa mechi hiyo pamoja na viongozi wa klabu ya SC Kiyovu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako