• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalam asema vita ya kibiashara itayaathiri zaidi makampuni ya Marekani

    (GMT+08:00) 2018-05-03 17:50:13

    Mkuu wa utafiti wa China katika shirika la kimataifa la MSCI Wei Zhen amesema, kampuni na wawekezaji wa Marekani wataathirika zaidi katika vita ya kibiashara inayoendelea kati ya China na Marekani.

    Kwenye waraka wake uliotolewa katika mtandao wa shirika hilo, Wei amesema asilimia 5.1 ya mapato ya kampuni katika alama ya MSCI USA inatoka China, na inaweza kuwa hatarini ikiwa ni matokeo ya vita ya kibiashara. Amesema kwa kulinganisha, ni asilimia 2.8 tu ya mapato ya kampuni katika alama ya MSCI China inayotoka Marekani.

    Amesema ingawa kupanuka zaidi kwa vita ya kibiashara kunaweza kusababisha hasara kwa pande zote mbili, biashara nchini Marekani zinaweza kuathirika zaidi kwa kuwa zinategemea sana uchumi wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako