• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Bei ya makaa na umeme yapanda

    (GMT+08:00) 2018-05-03 18:07:00

    Bei ya makaa na umeme imeendelea kupanda mwezi huu licha ya kushuka kwa jumla ya gharama ya maisha kwa mujibu wa data kutoka kwa shirika la takwimu.

    Shirika la kitaifa la takwimu (KNBS) limegundua bei ya mkebe mmoja wa makaa imefikia shilingi 125.48 kutoka kwa shilingi 80 mwezi mmoja uliopita.

    Bei ya makaa imepanda maradufu katika mda wa miezi 6 iliyopita kufuatia marufuku ya biashara ya makaa na ukataji miti iliyotolewa na waziri wa mazingira Keriako Tobiko.

    Kwa sasa gunia moja la makaa linauzwa shilingi 2500 kutoka 1500 katika sehemu nyingi jijini Nairobi.

    Kabla ya ongezko hilo makaa mkebe mmoja yaliuzwa shilingi 35 .

    Bei ya stima nayo ilipanda kwa asilimia 26.3 kutoka 590 kwa units 50 hadi 745.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako