• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Bandari ya Mombasa yapokea meli kubwa zaidi katika historia yake

    (GMT+08:00) 2018-05-03 18:07:45

    Moja ya meli kubwa zaidi ya mizigo duniani ilitua nanga katika bandari ya Mombasa wiki hii ikiwa ishara tosha kwamba shughuli za upanuzi wa bandari hiyo zilifanikiwa.

    Meli hiyo ya MV MSC kutoka Ureno iliwasili bandarini na kuvutia maelfu ya watu walioshangazwa kwa ukubwa wake.

    Kwa mujibu wa shirika la masuala ya bandari,meli hiyo ilibeba makonteina elfu 6 ya futi 20 na ina uwezo wa kubeba mizgo ya tani elfu 74 .

    Meneja wa oparesheni wa meli hiyo William Ruto amesema ujio wa meli hiyo bandarini Mombasa umedhihirisha kwamba bandari ya Mombasa imefikia viwango vya kimataifa kwani baada ya shughuli za kuchimba na kupanua maji ya bandari ya Mombasa meli zote kubwa sasa zinaweza kuingia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako