• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania;Serikali kuanzisha vita rasmi dhidi ya uvuvi haramu

    (GMT+08:00) 2018-05-03 18:08:42

    Bunge limeunga mkono vita dhidi ya uvuvi haramu iliyotangazwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kutaka viongozi wa ngazi zote wanaoshiriki au kufadhili uvuvi haramu watajwe kwa majina ili Taifa liweze kuwafahamu.

    Hali hiyo itasaidia kumaliza kabisa tatizo la uvuvi haramu lililosababisha nchi ishindwe kunufaika na rasilimali hizo muhimu za uvuvi licha ya kuwa na eneo kubwa la maziwa, mito na bahari lenye jumla ya kilomita za mraba 346,337 sawa na asilimia 36.7 ya eneo lote la Tanzania ni maji.

    Wakichangia mjadala katika semina kwa wabunge kuhusu vita dhidi ya uvuvi haramu iliyoandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kufanyika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni jijini Dodoma jana, baadhi ya wabunge waliitaka serikali kuchukua hatua kali zaidi kwa watu wote wanaojihusisha na kufadhili uvuvi haramu ili nchi iweze kunufaika na rasilimali hiyo muhimu.

    Aidha katika operesheni inayoendelea maarufu kwa jina la 'Operesheni Sangara 2018 ' jumla ya nyavu haramu zenye urefu wa mita milioni 34 zimekamatwa na kuteketezwa kwa moto, nyavu hizo zimekamatiwa katika maeneo mbalimbali ya ziwani, mipakani, madukani, kwenye maghala na viwandani.

    Alisema jumla ya kilo 310,569 za samaki zilizokuwa zimevuliwa kwa njia haramu na kinyume cha sheria zimekamatwa na kutaifishwa na serikali kati ya samaki hao jumla ya kilo 132, 325 za samaki wachanga na wazazi zimegawiwa kwenye hospitali, shule, magereza na wananchi na pia kilo 178,244 za kayabo na kilo 4,967 za mabondo zimeuzwa kwa njia ya mnada na fedha kuingia kwenye mfuko wa serikali.

    Akielezea kuhusu ukwepaji mkubwa wa kodi za serikali, Waziri Mpina alisema kwa kipindi kirefu serikali imekuwa ikipata kiasi kidogo cha mapato kutokana na biashara ya mazao ya uvuvi ambapo inakadiriwa kuwa chini ya asilimia 25 ya kiasi cha mapato inayostahili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako