• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Kenya: Migne wa Ufaransa achaguliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa 'Harambee Stars'

    (GMT+08:00) 2018-05-04 08:54:33

    Shirikisho la mpira wa miguu nchini Kenya limemtangaza Sebastien Migne wa Ufaransa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa 'Harambee Stars' na anachukua nafasi iliyoachwa wazi tangu mwezi februari na Paul Putt wa Ubeligiji.

    Migne mwenye umri wa miaka 44 amesaini mkataba wa miaka minne kuifundisha timu hiyo ambayo ndiyo mabingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati kwa sasa na jukumu lake kubwa la kwanza itakuwa ni kuisaidia timu hiyo kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa mwaka 2021.

    Kabla ya uteuzi huu, Migne alikuwa kocha mkuu wa timu ya vijana ya DRC, na anakuwa mkufunzi wa tatu kutoka Ufaransa kuwahi kuifundisha Harambe Stars baada ya Bernard Lama na Henri Michel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako