• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makubaliano kadhaa yapatikana katika mazungumzo ya masuala ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-05-04 17:28:11

    Naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He amefanya mazungumzo na ujumbe wa Marekani unaoongozwa na mjumbe maalumu wa rais wa Marekani ambaye pia ni waziri wa fedha Bw. Steven Terner Mnuchin tarehe 3 na 4 Mei.

    Pande hizo mbili zimefanya majadiliano yenye uwazi, ufanisi na wa kiujenzi kuhusu suala la kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani. ia zimekubaliana kuwa, kuna umuhimu mkubwa wa kukuza uhusiano tulivu wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili, ili kutatua masuala yanayohusika kwa kupitia mazungumzo. Pia zimebadilishana maoni juu ya kupanua uuzaji wa bidhaa za Marekani nchini China, biashara ya utoaji wa huduma kati ya pande hizo mbili, uwekezaji, kulinda hakimiliki ya ujuzi, na utatuzi wa suala la ushuru wa forodha na ule usio wa forodha, na kufikia maafikiano katika sekta kadhaa. Vilevile zimetambua kuwa bado ipo mikwaruzano mikubwa katika baadhi ya masuala, na inahitaji kuharakisha mchakato wa mazungumzo ili kupata maendeleo makubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako