• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya yatetea uamuzi wa kuanzisha huduma za mabasi ya usafiri wa umma

    (GMT+08:00) 2018-05-04 17:46:58

    Serikali ya Kenya imetetea uamuzi wake wa kushiriki biashara ya uchukuzi wa umma jijini Nairobi kupitia Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS),ikisema inalenga kusaidia Wakenya wanaoshindwa na gharama ya juu ya nauli, huku ikipanga kuongeza mabasi mengine 50.

    Hata hivyo, hatua hiyo imepingwa vikali na Chama cha Wamiliki wa Matatu kupitia kwa mwenyekiti Simon Kimutai, ambaye ameelezea hofu kuwa lengo la serikali ni kuangamiza sekta ya kibinafsi.

    Alitaka kujua ikiwa mabasi hayo yamefuata utaratibu sawa na wamiliki wa kibinafsi katika kupata leseni, huku akielezea kuwa nauli wanayotoza inajumlisha mambo mengi ya uwekezaji huo.

    Waziri wa Utumishi wa Umma, Vijana na Jinsia, Prof Margaret Kobia alisema walianzisha 'Operesheni Okoa Abiria' kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, na kusababisha nauli za matatu kupanda maradufu na kuwafanya Wakenya wengi kukwama kwa vituo vya mabasi.

    Mabasi hayo ya NYS, waziri alisema, yanatoza nauli ya Sh20, na hawangazii uundaji wa faida, bali tu kuweza kupata fedha za mafuta ya kuyawezesha kuhudumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako