• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wataalamu wa sekta ya ujenzi wasdsema nyumba za bei nafuu zitainua uchumi

    (GMT+08:00) 2018-05-04 17:47:26

    Wataalamu wa sekta ya ujenzi na uwekezaji nchini Kenya wamesema uchumi wa taifa huathirika vibaya kutokana na uhaba wa nyumba bora zinazoweza kumudiwa na idadi kubwa ya wananchi.

    Wakizungumza kwenye kongamano la uwekezaji na ujenzi jijini Nairobi walisema wanatumai serikali itafanikiwa kutekeleza mipango yake ya kujenga nyumba za bei nafuu kwa wananchi kabla Rais Uhuru Kenyatta ahitimishe muhula wake wa pili uongozini.

    Mkuu wa mikakati maalum katika Benki ya Barclays Moses Muthui alisema wanatathmini kwa kina kuhusu nyumba za bei nafuu na jinsi wanavyoweza kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa ajenda kuhusu makao,chini ya nguzo nne kuu za maendeleo.

    Kulingana na wataalamu wa masuala ya kiuchumi,wananchi wengi hasa jijini Nairobi hutumia sehemu kubwa ya mapato yao kulipa kodi za nyumba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako