• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kupunguza zaidi ushuru kwa makampuni madogo na ya tenkolojia za hali ya juu

    (GMT+08:00) 2018-05-04 18:31:43

    Mkutano wa baraza la serikali ya China uliofanyika hivi karibuni umeamua kutekeleza hatua saba kupunguza ushuru wa zaidi ya renminbi yuan bilioni 60 sawa na dola za kimarekani 9.45, haswa kwa makampuni madogo na ya teknolojia za hali ya juu.

    Naibu waziri wa fedha wa China Bibi Cheng Lihua jana kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, madhumuni ya hatua saba za kupunguza ushuru kwa makampuni ni dhahiri, ya kwanza ni kupunguza gharama za uendeshaji wa makampuni madogo, ili kuwahamasisha watu wengi zaidi kuanzisha makampuni; ya pili ni kuunga mkono makampuni kuboresha vifaa na kuongeza mafunzo kwa wafanyakazi wao, ili kuongeza uwezo wa uvumbuzi.

    Bibi Cheng amesema hatua hizo zinalenga kuongeza nafasi ajira, kwani nchini China kuna idadi kubwa ya makampuni madogo, na makampuni hayo yanawaajiri wafanyakazi wengi. Bibi Cheng anasema,

    "Kwa mfano sasa tunatoza ushuru makampuni madogo kuanzia mapato ya yuan milioni moja badala ya laki tano za zamani, na pia tumepunguza kiwango cha ushuru huo kuwa asilimia 10 kutoka 20. Aidha tumeeneza majaribio ya kupunguza ushuru wa makampuni madogo kote nchini China, na kuyasaidia makampuni hayo kupata uwekezaji. Hatua hizo zitahamasisha watu kuanzisha makampuni, na kuongeza nafasi za ajira."

    Bibi Cheng amesema kuhimiza uvumbuzi pia ni lengo muhimu la China katika kutekeleza hatua za kupunguza ushuru. Hadi sasa China imekamilisha mfumo wa kupunguza ushuru wa makampuni ya teknolojia za hali ya juu. Bibi Cheng anasema,

    "Kwa mfano tumeongeza muda wa makampuni ya teknolojia za hali ya juu wa kuwianisha hasara na mapato kuwa miaka 10 kutoka mitano. Pia tumeongeza gharama za mafunzo kwa wafanyakazi ya makampuni hayo kuwa asilimia 8 ya mapato kutoka 2.5 ambayo zinasamehewa ushuru."

    Bibi Cheng amesema wizara ya fedha, idara kuu ya ushuru pamoja na idara nyingine husika za China zitaharakisha kuandaa nyaraka za kutekeleza rasmi hatua hizo, ili kunufaisha kihalisi makampuni madogo na ya teknolojia za hali ya juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako