• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China azungumza na viongozi wa Japan na Korea ya Kusini kwa njia ya simu

    (GMT+08:00) 2018-05-04 21:08:04

    Rais Xi Jinping wa China leo kwa nyakati tofauti amezungumzo na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na rais Moon Jae-in wa Korea Kusini kwa njia ya simu.

    Alipozungumza na waziri mkuu wa Japan, rais Xi amesema huu ni mwaka wa 40 tangu China na Japana zisaini mkataba wa amani, nchi hizo mbili zinapaswa kufuata mkataba huo, na kudhibiti migongano ili kuhakikisha uhusiano kati yao unarejea katika njia ya kawaida na kupata maendeleo zaidi. Kwa upande wake, Shinzo Abe amesema Japana inatilia maanani uhusiano kati yake na China, na kupenda kuboresha na kuendeleza uhusiano huo.

    Katika mazungumzo yake na rais Moon wa Korea Kusini, rais Xi amesema, hivi sasa uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendelea kwa utulivu, China inapenda kuongeza mawasiliano na Korea Kusini ili kuhimiza uhusiano huo uendelee katika mwelekeo unaolingana na maslahi ya nchi hizo mbili. Naye rais Moon amesema Korea Kusini inajitahidi kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati yake na China kuendelea zaidi, na kutaka kuongeza mawasiliano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako