• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yang Jiechi na Mike Pompeo wajadili suala la Peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2018-05-06 16:21:38

    Mjumbe wa ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Yang Jiechi amezungumza na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kwa njia ya simu wakibadilishana maoni kuhusu suala la Peninsula ya Korea.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema Bw. Yang Jiechi ambaye pia ni mkurugenzi wa Ofisi ya Tume ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC amesema katika mazungumzo yao, Bw. Yang ameeleza msimamo wa upande wa China wa kushikilia kufanya Peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na silaha za nyuklia, kushikilia kulinda amani na utulivu wa Peninsula hiyo na kutatua masuala husika kwa njia ya mazungumzo na mashauriano.

    Bw. Yang pia amezitaka pande mbalimbali zifanye jitihada za kudumisha mwelekeo mzuri wa utatuzi wa suala la Peninsula hiyo na kuangalia kwa uwiano ufuatiliaji wa pande zote katika mchakato wa kusukuma mbele uondoaji wa silaha za nyuklia katika Peninsula hiyo ili kuifanya iwe sehemu yenye utulivu wa kudumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako