• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka makampuni ya kigeni nchini humo kuheshimu mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China

    (GMT+08:00) 2018-05-06 19:29:08

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema makampuni ya kigeni yaliyomo nchini humo yanatakiwa kuheshimu mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China.

    Hivi karibuni, Marekani ilitoa taarifa ikikosoa hatua ya China ya kutaka makampuni ya kigeni kutofanya sehemu za Hong Kong, Macao na Taiwan kuwa "nchi" katika tovuti na nyaraka zao.

    Msemaji huyo amesema kuwa, duniani kuna China moja tu, na Hong Kong, Macao na Taiwan ni sehemu zisizotengeka kutoka ardhi ya China, hii haiwezi kubadilika bila kujali kuwa Marekani inasema nini. Ameongeza kuwa China itaendelea kushughulikia uhusiano na makampuni ya kigeni kwa kutumia kanuni za kuwepo kwa China moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako