• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China iko tayari kuhimiza mazungumzo na amani katika Mashariki ya Kati

    (GMT+08:00) 2018-05-07 10:01:46

    Mjumbe maalumu wa China anayeshughulikia suala la Mashariki ya Kati Bw. Gong Xiaosheng, ameeleza wasiwasi kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, akisema China itafanya juhudi kuhimiza mazungumzo na amani katika sehemu hiyo.

    Bw. Gong Xiaosheng amesema hayo wakati wa mazungumzo kati yake na ofisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia anayeshughulikia mambo ya kisiasa na kiuchumi Bw. Jamal Aqeel.

    Bw. Gong amesema masuala mbalimbali yakiwemo vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, migogoro kati ya wapalestina na waisraeli, vita nchini Yemen, na migongano kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Iran vinahatarisha amani na utulivu wa Mashariki ya Kati, hali ambayo inafuatiliwa sana na China.

    Pia amesisitiza kuwa China iko tayari kuhimiza mazungumzo na amani ili kutatua masuala hayo haraka iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako